Warning: Missing argument 2 for wpdb::prepare(), called in /hermes/bosweb25b/b1244/ipg.amayabeautyspacom/wp-content/themes/limon/functions/includes/po.php on line 125 and defined in /hermes/bosweb25b/b1244/ipg.amayabeautyspacom/wp-includes/wp-db.php on line 990

Warning: Missing argument 2 for wpdb::prepare(), called in /hermes/bosweb25b/b1244/ipg.amayabeautyspacom/wp-content/themes/limon/functions/includes/po.php on line 201 and defined in /hermes/bosweb25b/b1244/ipg.amayabeautyspacom/wp-includes/wp-db.php on line 990

Select a page

Jun 11th

Utunzaji Nywele na Stylist

Posted by with No Comments

                         FAHAMU NYWELE ZAKO KABLA HUJAMPA KICHWA STYLISTS.

      Topic yetu ya leo ni kujaribu kuwafundisha wateja wetu, na wasio wetu, umuhimu wa kujua nywele zao kabla aujampa stylist kichwa chako. Inawezekana mapungufu ya stylist hutokana na ufinyu wa vifaa kwenye salon wanayofanyia kazi,(ukigundua hilo hima hima tafuta vitu vyako) lakini pia inawezekana huyo stylist bado ni mgeni wa kufanya kazi au amesoma siku nyingi (haendi na wakati) au amejifunzia barabarani ama  sababu nyengine  nyngi  tunazozifahamua. Hakuna tatizo, la muhimu ni kwamba wewe ndio unaejua matatizo ya nywele zako kabla hujaomba msaada wa kuyatatua kutoka kwa professional wa nywele.

Sasa briefly tutakupa mafunzo ya jinsi nywele zako zinavyotakiwa kutibiwa ili ukiona stylist anafanya visivyo, unaweza kumshtua na kumpa matakwa yako.

 Kuwa muangalifu jinsi  stylist wako anayoosha Nywele. 

       Mara nyinigi tumeona stylists wanasugua sana ngozi ya mteja kwa  kuamini kuwa hivyo ndivyo usafishaji wa nywele na ngozi, unavyotakiwa, inaweza kuwa sawa, theoritically  bt kuna madhala yake makubwa sana pale nywele au ngozi inaposuguliwa kwa nguvu.

Moja ya madhala ni udhoofishaji wa  uhusiano kati ya nywele na ngozi. Na ni sababu moja wapo ya ukatikaji wa nywele. Kukanda ngozi yako ni vizuri zaidi na hakukati nywele kabisa na kunafanya u  relax muscles za kichwa chako.

Stlist anatakiwa kutumiai vidole vyake na  viganja kuosha nywele zako, vidole viwe vinasugua ngozi polepole na viganja vinakanda kichwa, kwani uoshaji wa nywele salon ni moja ya mawasiliano kati yako wewe na stylist wako na mahitaji ya nywele zako. (Hii tunafanya vizuri sana Amaya, au sio wateja wetu).

 Beba products zako kama huna uhakika ( hili kwetu amayaBSS hatuna wasiwasi vitu vyetu ni Original):

       Wengi au wote tunafahamu kwamba kwa sasa Tanzania tumeingiliwa na vitu fake vingi sana. hususan kwenye ma salon. Sababu ni nyingi, lakini moja wapo ni ya bei za  bidhaa za vitu originals,  na prices za wateja wanazozitaka. Salon nyingi zinashindwa ku afford kununua  vitu original, na wengi wetu hawajui tofauiti kati ya original na fake ( wachina kiboko;) but  (hii ni topic  nyengine kabisa  tutaongea siku nyengine.) hii inasababisha madhala makubwa sana katika nywele na vitu vyengine vingi sana katika miili yetu. But leo tunaongelea nywele ngoja turudi kule. Sasa kama unaona nywele au ngozi yako iimekuwa kavu sana kuliko kawaida,  na nywele zimekuwa  ngumu sana baada tu  ya kuoshwa, mara nyingi inakuwa nywele zimewekwa  wrong shampoo au conditioners(hii nayo ni makala mpya kabisa kuhusu type za shampoos) point yetu hapa kama una wasiwasi na product anazotumia stylist wako, ni bora uende na products zako mwenyewe kuepusha madhala ya baadae.

 

Tumia Taulo kukaushia nywele kwa muda zaidi kuliko Moto:

      Mara nyingi sana stylists wanatumia muda mfupi sana kukausha nywele na taulo, wanakukimbiza kwenye blow driers, au flat iron, or drier kwasababu wanazozijua wenyewe. Inashauriwa kutotumia heat sana kukaushia nywele zako. Ni vizuri zaidi kutumia taulo au hewa ili nywele ziwe na rutuba zaidi.   heat ina madhala makubwa saa kwenye nywele, kwanza zinadhoofisha nwele, zinafanya nywele ziwe na split end na mbaya zaidi heat inakata sana nywele. kwahiyo zingatia sana  muda mfupi kwenye drier, ina maana muda mfupi kwenye moto na ndio furaha za nywele zako.

Kitu kingine cha muhimu ni kuwa mungalifu sana na  stylist wako pale anavyo kausha nywele hatumii nguvu kusugua nywele zako na taulo bali  ana squeeze nywele zako polepole na taulo,  usuguaji wa nguvu  na taulo unasababisha ukatikaji wa nywele.

 

Kuwa Mwangalifu Unapochanwa Nywele:  

     Kuna uwezekano mkubwa sana  kwako kuavoid kukatika kwa nywele zako pindi pale utakapozingatia na kuangalia  jinsi  gani  stylist anachana nywele zako. Muhimu ni kuangalia jinisi anavyoshika nywele zako kabla hajanza kuzichana.  kwanza anatakiwa ku” detangle” , kuzichambua nywele zako kabla ya  kuzichana, wengine wanaanza tu bila kuzichanbua, ni makosa, kwani wakati huo nywele zako ni mbichi na ngozi yako imefunguka kwasababu ya kuoshwa, na kukandwa, inabidi ichukuliwe polepole. kama unaona stylist anaanza vibaya usisite kumwambia,  kumbuka hizo ni nywele zako na unalipa kwa service yao.  Kwahiyo usiogope kusema kama stylist hakufurahishi na uchanaji wa nywele zako.

 Kumbuka mambo haya machache uchanapo nywele na stylist:

  •  Achambue nywele zako ktk section ndogo ndogo akitumia kitana chenye ncha kubwa, ili aweze kuzichambua kirahisi.  Vitana vyenye mapana madogo vinakata sana nywele, especially kama  nywele zako zina maji. (kama huna uhakika na vitana vya salon unayoenda, nenda na vyako) lesson ya aina ya  vitana nayo  itakuja very soon
  • Nywele zisichambuliwe zikiwa zimeloa tepe tepe,  kwani pale ndipo muda nywele zako ziko very weak na  rahisi kukatika, hakikisha nywele zako amezikausha vizuri sana na taulo kama tulivyosema mwanzo , kabla hazijachabuliwa.
  • Anaweza kuweka leave in conditioners au mafuta/serum, kulainisha nywele wakati wa kuchanwa, hii inaweza kuku cost more ukiwa salon,  lakini utaona mafanikio yake palepale wakati nywele zako zinachanwa
  • Stylist anatakiwa kushika nywele kutoka kweye roots, wakati wakichambua ili waweze kuchana bila kuumiza ngozi yako na  kuzuia ukataji wa nywele zako.
  • Hakikisha  anazichambua kutoka chini kwenda juu, sio juu kwenda chini.

 

 Jinsi ya ku blow dry kwa usahihi:

     Kwa  wale wenye dawa, au nywele ambazo hazina dawa, hata siku moja zisikaushwe na drier yenye moto mkali.  Mara nying sana stylists wanachagua kufanya hivyo kwani ndio njia pekee ya kufanay nywele kuwa laini haraka ili iwe raisi kwao kuzinyoosha mapema. Hata kama ni rahis kwao, zingatia kwamba si kitu kizuri kwenywe nywele zako kwasababu zinafanya nywele zako ziwe kavu na weak zaidi, hasa zinafanya ncha za mwisho za nywele zako, (split end)  kukatika na  nywele kuonekana hazina rotuba.

Pia zingatia sana ukaribu anaouweka kati ya nywele zako na drier, isizidi kati ya 6-8 inches, ukiona ngozi yako imekaza sana au inavuta baada ya kukaushwa, ina maana drier ilikuwa karibu sana  au ilikuwa na moto mkali sana au sababu zote mbili.

 

Kuwa Mwangalifu sana na matumizi ya Spritz’s na Serum.

     Ni kweli kabisa tunapenda sana tukae na style tulizo tengenezwa salon kwa muda mrefu kidogo, yaaah, tumetumia pesa zetu au sio, Hapo ndipo stylist anapoweka sritz after spritz after spritz, ili nywele zikae pahali pake bila kuaribiwa na upepo au kitu chochote. hizi sprays zinasaidia sana, lakini matumizi yake kwa muda mrefu yana madhala makubwa sana katika nywele zetu, kwasababu ya  amount ya alcohol iliyopo kwenye hizo products, zinafanya nywele  kukauka sana na kuharibu volume ya nywele zako na kukata kabisa nywele.  Serum nayo nia adui wetu akitumiwa kwa wingi, kazi maalum ya serum ni kufanya nywele zinga’ae na  kulainika kidogo, syrum nyingi ina attract uchafu, hasa  vumbi letu hili la dar,  na inafanya nwele zichafuke na kusababisha mba. Kama unataka kuwa na nywele zenye afya  na zenye rutuba, hakikisha  unaongea na stylist  wako ili athamini  nywele zako kama unavyozithamini wewe na kuweka products chache au zinazotosheleza kuliko kuzi over feed mambo yasiyoitajika.

 

                                                                            kuwa mwangalifu na Moto unaowekwa kichwani:

 

       Well kwa kweli wakati mwengine  nywele zetu zinaitaji sana moto ili zikauke vizuri, wakati mwengine naskia wateja wanalalamika sana “oooh mbona hii drier haina moto”, mara ” sina muda nataka kuondoka nimetoroka ofisini mara moja”!!! Heat ni muhimu sana katka urembo wetu, lakini tukumbuke moto sio kitu kizuri sana kwa nywele zako, hasa kama unataka nywele zako zidume na zikue, lazima uangalie sana stylist wako anatumiaje moto katika kichwa chako.  Bahati mbaya sana huwezi kujua kwa uhakika kabisa chuma kina moto kiasi gani mpaka hapo kitakapofikia kwenye kichwa chako, lakini unaweza kuona hizi  signs ambazo utajua huo moto haouko sawa:

  • Kwanza utaanza kuona sehemu ya nywele zako nchani au mwishoni kuonekana zimenyooka sana wakati nywele zako zimelowa.
  •  Utaona nywele zako zinaanza kuwa nyembamba na chache, hasa area za mbele ya uso wako.
  •  Nywele pia zitakuwa zimepauka na ngumu kidogo zikishikwa, ugumu wake ule ni matokeo ya matumizi mabaya ya drier kwenye nywele zako na utumiaji mbaya wa products zenye alcohol nyingi kwenye nywele zako kama vile spritz,

  Hakikisha kitana cha moto kinasafishwa Mara kwa Mara:

        Hii ni muhimu sana kwani kinatumika sana na kinaunguza nywele mara kwa mara, kikiwa kisafi kitafanya kazi nzuri kunyoosha nywele zako vizuri  zaidi, na hazitaziharibu nywele zako, kama uki notice nywele zako zinanuka harufu usioilewa baada ya kumaliza, maana yake vile vifaa  amabavyo  wamevitumia vilikuwa vichafu kabla hawajakutengeneza nywele zako.

 

Haya Kina  dada, maada hii I hope itawasaidia sana kutunza nywele zenu kabla haijafika siku ambayo unaanza kutafuta mafuta ya kukuza nywele. Na kwa wale ambao kwa sasa wapo kwenye  matumizi ya yale mafuta yetu ya jukuza nywele tena,  atleast  kwa sasa wanajua wamefikaje hapo na wafanyaje sasa ili wasifike huko tena . Asanteni sana na nawatakia utunzaji mwema wa nywele zenu. Karibuni sana  Amaya BSS kwa mafunzo na utunzaji wa nywele zako zaidi.

 

 

Picture courtesy of iclip, amaya Bss, google image.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *